Breaking News: HABARI MPYA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE KUTOKA KLABU YA YANGA IKIWA UGENINI SHELISHELI

Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga imefanya mazoezi yake ya mwisho asubuhi ya leo kwenye Uwanja wa Stade Linite utakaotumia kwa mechi ya kesho dhidi ya St. Louis.

Yanga ilifanya mazoezi hayo kuanzia mapema saa 3 asubuhi na kumalizika saa 5 kasoro.

Katika mazoezi hayo, wachezaji walianza kwa kupasha miili joto kabla ya benchi la ufundi kuwagawa timu mbili kwa ajili ya kucheza uwanja mzima.

Katika mazoezi hayo, kiungo Kabamba Tshishimbi alikuwa kivutio kutokana na uwezo wake wa kuchezesha timu na kutawala eneo la kiungo.

Mshambuliaji Juma Mahadh hakuhudhuria mazoezi hayo kutokana na kutokuwa sawa kiafya, wachezaji wengine wote walihudhuria tayari kwa mechi hiyo.

Yanga wanahitaji sare ya aina yoyote au ushindi ili kujihakikishia kusonga mbele katika mashindano hayo makubwa kwa hatua ya klabu barani Afrika

Post a Comment

0 Comments

Close Menu