Kocha msaidizi wa Simba Mrundi Irambona Masoud Djuma akiongea na kituo cha radio hapa chini amethibitisha kwamba golikipa wao Aishi Manula atakuwepo langoni katika mchezo wa marudiano wa Caf Confederation Cup dhidi ya Gendarmerie leo jioni
Manula aliumia mkono wa kushoto jana katika mazoezi ya mwisho na ikaelezwa huenda akaukosa mchezo wa leo kutokana na maumivu hayo.
Kocha huyo ametaja jina la nahodha wa kikosi hicho John Bocco kuwa yeye peke ndiye atakayeukosa mchezo huo kutokana na majeraha aliyopata kwenye mchezo wa lig dhidi ya Mwadui Fc.
“Aishi yuko vizuri watanzania wote wajue, kweli jana alipata tatizo mazoeni lakini yuko vizuri na atacheza mechi, wapenzi wa Simba waache wasisi wazidi kutuombea tufanye vizuri.”
“Wachezaji wote wako tayari isipokuwa nahodha John Bocco ndiyo atakosekana lakini wengine wote watakuwepo kwa ajili ya kupambana kwa ajili ya mechi ya leo. Tunajua sio kazi rahisi lakini tutapambana kama kawaida yetu mwanzo wa mechi hadi mwisho tuhakikishe Simba inasonga mbele.” alimaliza kocha huyo mwenye mbwembwe nyingi uwanjani.
0 Comments