Beki wa Yanga, Andrew Vincent 'Dante' amesema mpaka sasa bado ubingwa wa Ligi Kuu Bara hauna mwenyewe na kwamba kikosi chao kina mpango maalum wa kuwakimbiza vinara wa ligi hiyo Simba.
Dante alisema kitendo cha Simba kupata sare isioyotarajiwa wiki iliyopita kiimewapa morali Yanga na kwamba sasa wanataka kushinda katika kila mchezo.
Beki huyo aliyesajiliwa na Yanga akitokea Mtibwa Sugar mwaka mmoja na nusu uliopita alisema kwa sasa kikosi chao kinatakiwa kujiimarisha na kuhakikisha kinashinda mechi zao bila kuiangalia Simba.
Alisema kupitia sare ambayo Simba imeipata watakuwa na presha katika kila mchezo watakaocheza jambo ambalo linaweza kuwakuta wakifanya makosa mengine.
"Tunanafasi ya kutwaa taji mpaka sasa halina mwenyewe muhimu ni kujipanga na kuhakikisha malengo yetu ya kushinda kila mchezo yanafanikiwa,” alisema Dante.
"Hakuna aliyetarajia Simba ingepata ile sare, lakini huku kwetu tuna mipango ya kushinda kila mchezo na sasa hatutakiwi kuangalia sana matokeo ya Simba muhimu ni kuhakikisha tunashinda mechi zetu na hilo linawezekana."
0 Comments